( Mpangilio wa
hema la kukutania).
"Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.
Kutoka 40: 1,2. Mungu alitaka Musa amjengee sehemu au mahala pa kukutana.
"Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia" Walawi 1:1. Mungu anamuita Musa akimtaka aende mahala pa kusemezana/kukutana
ili aweze kusema naye. Kumbe ili tuweze kuongea na Mungu tunahitaji tutafute mahala rasmi na penye utulivu ili Mungu atusikilize na tumsikilize nini anataka kutoka kwetu.
TENT
OF MEETING ( Hema ya kukutania), Ni mahali ambapo umepaandaa na kuweka muda fulani rasmi
ili kuongea na kumsikiliza Mungu na Roho mtakatifu. Ni wewe mwenyewe unakutana na Mungu wako na
kuongea naye kama rafiki. Huu ni utaratibu wa kila siku kwa mkristu mkatoliki
kwani unakupa muda wa kutafakari maandiko kwa undani zaidi kwa msaada wa Mungu
na Roho mtakatifu.
"Njoo Roho Mtakatifu" - Ninaomba
msaada wa Roho Mtakatifu-kwa wimbo, sala fupi au kwa maneno yangu mwenyewe.
"Yesu yuko hapa" -Natambua kwamba
yuko hapa kweli , yeye yuko nami hapa na sasa.
"uso kwa uso, kama mtu anayesema na
rafiki" - ni kukutana na marafiki ambao wote wanafurahi kukutana na naweza
kuonyesha furaha yangu katika maombi ya ibada. Yesu ni rafiki yangu, anafurahi
kuwa pamoja nami, ananipenda, ananijali - ni kama kuwa nimekubaliwa naye.
"Sema, BWANA, kwakuwa mtumishi wako
anasikiliza" - Bwana anataka kuniambia kitu fulani mahala hapa na sasa. Ni
sala ya neno kwangu.
"Bwana, nifanye nini?" - Katika hali ya amani ya ndani, ninakaa kimya na
kutafakari mitazamo. Ninaanza kudadisi ndani yangu-napenda kusikia kile Yesu
anataka kuniambia leo.
"Neno lako ni taa ya miguu yangu" -
sasa nisoma kifungu kilichochaguliwa na kilichoandaliwa kutoka kwenye Biblia -Ninasoma
polepole na kwa uelewa- unaweza kurudia mara kadhaa.
"Sauti nyepesi ya ukimya" -Nabaki
kimya, nikisubiri na kusikiliza kwa makini sauti ya Mungu-kwa uvumilivu na
imani. Ni kukutana na Mungu katika mawazo yangu, moyo wangu na kumbukumbu zangu.
"Kwa
malaika. . . andika hili. . . " - Ninaandika katika daftari yangu
ndogo mawazo ambayo yamekuja katika akili yangu- kuyaokoa ili yasisahaulike na kuyarudia
pindi nitakapo hitaji.
"Bwana. . . Ninaamua sasa. . . " - Ninafanya azimio na ninaandika katika
daftari langu dogo – kama tu kwa uwazi linatokea ndani yangu, sijilazimishi
kufanya azimio, kwa sababu sio msingi wa hema ya kukutania.
"Asante Yesu" -Namshukuru Mungu kwa
kukutana na kwa neno lake. (Unaweza pia kukabiliana na fadhili za Mungu kwa
kutubu kweli kutoka moyoni, lakini si lazima .. Sala inapaswa kuishia kwa
shukrani.).
This is how we speak to Lord, I usually talk to him and ofcourse I observe many thing which I have never seen coming from God directly. Try to have two days for Tent of Meeting you shall believe me
ReplyDeleteAmen, that is. i agree with you. we need time to talk with God. and he He needs us ( you personally as friend )
ReplyDeleteonline casino【VIP】Play blackjack online
ReplyDeleteOnline 온라인 카지노 대한민국 casino【VIP】Play blackjack online.【WG98.vip】⚡,blackjack online casino,casino,online poker room,blackjack poker,golf game,