Wednesday

Maana ya Light-life Movement















Light-life movement ni moja ya harakati za upya katika Kanisa Katoliki. Ina mizizi yake katika mafundisho ya mkutano mkuu wa pili wa Vatican na imeidhinishwa na maaskofu. Light-life movement hukusanya pamoja watu wa rika zote na majukumu mbalimbali, (watoto, vijana, watu wazima, familia, makuhani, watawa na wanachama wa taasisi za kidunia. Light-life Movement ni msaada bora kwa mkristu katika mafundisho na Imani ndani ya kanisa Katoliki, na zaidi mno katika safari ya kwenda Mbinguni kwa Mungu Baba. 
Alama au maneno yaliyopo kwenye Msalaba ni alama ya Kikristo ya awali phos-zoe (maneno ya Kigiriki yenye maana ya mwanga na maisha yaliyojiunga na herufi ya omega na kutengeneza msalaba). Ishara hii inaonyesha kanuni kuu ya maisha ya Kikristo - umoja wa imani na maisha.




No comments:

Post a Comment

God Bless You